Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akimtwisha ndoo ya
maji Bi. Diana Salum mkazi wa Kata ya Kilongo Manispaa ya Morogoro baada
ya kuzindua moja ya visima 23 virefu vya maji vilivyochimbwa na mbunge
wa jimbo hilo Mohammed Aziz Abood,
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akifungua bomba la maji mara baada ya kuzindua kisima hicho leo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akikata utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa kisima cha maji katika kata ya Kilongo
Manispaa ya Morogoro, kulia ni Mohammed Aziz Abood Mbunge wa jimbo la
Morogoro mjini na kushoto ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Kata ya Kilongo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na
wananchi katika kata ya Kilongo kushoto ni Mbunge wa Morogoro Mjini
Mohammed Aziz Abood
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akifungua bomba la maji mara baada ya kufungua kisima cha maji katika kata ya Kichangani, kulia ni Mbunge wa Morogoro Mjini Mohammed Aziz Abood.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdurahman Kinana
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye
uwanja wa shule ya Kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro mjini ,
mkutano huo ukikuwa ni wa kumalizia ziara yake ya siku nane ambapo
amezunguka katika wilaya zote za mkoa wa Morogoro.
Akizungumza
katika mkutano huo pamoja na mambo mengine amewataka wabunge wa CCM
kutembea kifua mbele kwani chama chao kimefanya kazi kubwa lakini pia
bado wanayo kazi ya kuisimamia serikali ili itimize wajibu wake na
kwamba CHADEMA hawana uwezo huo zaidi ya kuifanya nchi
isitawalike.Kinana kwa madhamira yao siyo kuwatumikia wananchi bali
wanaangalia maslahi yao binafsi
Amesema
kitendo cha CHADEMA kushindwa kuwatumikia wananchi wamegeuka na
kuanzisha vurugu huku wakijaribu kuvuruga kila kitu kizuri ambacho
kinafanywa na serikali ya CCM kwa maslahi ya watanzania.(PICHA NA
KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG-MOROGORO)
Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano
huo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Jukwani.
Umati wa wananchi ukiwa umejitokeza kwa wingi katika mkutano huo uliofanyika mjini Morogoro leo. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond pamoja na wacheza shoo wake wakipagawisha wananchi katika mkutano huo.
Katibu wa NEC Oganizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib akizungumza katika
No comments:
Post a Comment