Wednesday, 4 December 2013

KINANA AENDELEA NA ZIARA KATIKA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbalizi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mahubiri katika mji wa Mbalizi, Kinana yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi akikagua  utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM  na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Ambapo leo ameendelea na  ziara yake katika wilaya ya mbeya vijijini, Abdulrahman  Kinana anafuatana na wajumbe wa halmashauri kuu ya  taifa Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye jana ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge wa katika bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania, Katibu mkuu huyo kesho anamalizia ziara yake kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe jijini Mbeya (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBALIZI -MBEYA VIJIJINI)2Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na uenezi  akiwahutubia wananchi wa Mbalizi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mahubiri.4Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo leo.5Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akizungumza na Dr. Norman Sigalla Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakati wa mkutano huo.6Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi akimkaribisha Ndugu Abdulrahman Kinana ili azungumza na wana Mbalizi.7Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakinyanyua mikono juu wakati mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa Zahanati katika kijiji cha Chamwengo Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya vijijini.2Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala leo.3Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala wakiwa katika ujenzi wa zahanati hiyo leo.4Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala  akiliweka sawa tofari wakati akishiriki ujenzi wa zahatati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala leo.5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua tanki la maji linalojengwa katika kijiji cha Itimu kata ya Iwindi Mbeya vjijini.6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na mjumbe mmoja wa mabalozi wakati alipokuwa akielekea kufungua shina la CCM mjini Mbalizi8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana  akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho wakati alipofungua moja ya matawi ya chama hicho mjini Mbalizi9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wananchama waliojiunga katika tawi hilo11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake pamoja na viongozi wenzake wakielekea kwenye mkutano wa ndani unaofanyika kwenye chuo cha ufundi Mbalizi12Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa tanki la maji katika mradi wa maji wa kata ya Iwindi wakati alipotembelea leo.

No comments:

Post a Comment