Friday, 6 December 2013

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI ABDULLAZIZ ABOOD AWATUNUKU VYETI WANAFUNZI WENYE VIPAJI WA KIDATO CHA SITA KILAKALA.

Mbunge wa jimbo la Morogoro Abdullaziz Abood akipokea risala kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha sita, Emiliana Shayo mara baada ya kusoma risala hiyo, kushoto ni mkuu wa shule hiyo Tabitha Tusekelege.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya vipaji kwa wasichana ya Kilakala, Dancan Kilimba akizungumza jambo wakati wa mahafali ya 47, kushoto ni Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood na kulia ni Diwani kata ya Kilakala kupitia tikiti ya CCM, Libon Mkali
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akipitia risala yake muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari wenye vipaji ya Kilakala wakati wa mahafali ya kidato hicho mkoani hapa, kushoto ni mkuu wa shule hiyo Tabitha Tusekelege na kutoka kulia niDiwani kata ya Kilakala kupitia tikiti ya CCM, Libon Mkali, Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya vipaji kwa wasichana ya Kilakala, Dancan Kilimba.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita kabla ya kunutukiwa vyeti na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood (mwenye kaunda suti ya blue) akimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha sita, Mary Axaud akimweleza jambo juu ya malighafi zinazotumika kutengeneza sababu ya maji wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya wanafunzi katika mahafali ya 47 ya kidato cha sita ya shule ya vipaji ya wasichana ya Kilakala mkoani hapa. kushoto ni mwalimu wa kidato cha sita wa somo la biology, Mzeru Paul.
Mwanafunzi wa kidato cha tano Ester Philimon (katikati) akimfafanua jambo kwa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullazziz Abood kulia wakati wa maonyesho ya kazi zinazofanywa na wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo la ICT PROGRAM IN KILAKALA muda mfupi kabla ya sherehe ya mahafali ya 47 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo. kushoto ni Maria Maganga na wa pili kutoka kulia ni Julieth Majura
Wanafunzi wa kidato cha mwanza hadi tano shule ya sekondari ya wasichana wenye vipaji ya Kilakala wakifurahia jambo wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari ya wenye vipaji Kilakala wakiingia ukumbini kwa ajili ya mahafali ya 47 yaliyofanyika shuleni hapo.
Wanafunzi wa shule ya vipaji ya wasichana ya Kilakala sekondari wakiwa na bango lenye kukaribisha wageni wakati wa mahafali ya 47 ya kidato cha sita mkoani Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood kushoto akisaini kitambu cha wageni katika shule ya vipaji ya wasichana ya Kilakala.

No comments:

Post a Comment