SETI YA MASHINE YA ULTRASOUND YENYE THAMANI YA SH 25 MILIONI
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya X-RAY Daktari Alban Ndekeye kulia na Daktari Paul Henry wa kitengo cha idara ya X-RAY wakati wa uzindua wa mashine ya ultrasound mpya yenye thamani ya sh25 milioni kwa ajili ya hospita ya rufaa ya mkoa Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullazziz Abood kizungumza jambo kabla ya kuzindua mashine hiyo, kulia ni
Dk Ritha Lyamuya
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Godfrey Mtei akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo, kutoka kulia ni Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Rutha Lyamuya na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullazziz Abood.
Mkuu wa Idara ya X-RAY Daktari Alban Ndekeye akizungumza jambo kuhusu mashine hiyo.
Sehemu ya viongozi wa idara mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
WAANDISHI wa habari Lilian Lucas na Josephine Malango.
NA LILIAN LUCAS, MOROGORO.
HOSPITALI ya rufaa ya mkoa wa Morogoro imepata mashine ya kipimo cha Utra-Sound yenye thamani ya shilingi 25 milioni baada ya zaidi ya miezi miwili kutokuwa na huduma ya mashine hiyo kwa wananchi ya mkoa wa Morogo.
Akizindua mashine hiyo hospitalini hapo jana mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdulazizi Abood aliwataka watumishi wa idara ya utra-sound na x-ray kutoa huduma kwa usawa kwa wananchi kwani kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwao.
Aboodi alisema huduma hiyo ni moja ya huduma zinazotegemewa na wananchi walio wengi,na kwamba katika kipindi hicho cha miezi miwili wananchi walikuwa wakipata huduma hiyo nje ya hospitali kwa gharama kubwa ambayo baadhi yao walikuwa wakishindwa kulipia gharama hiyo.
“Naupongeza uongozi wa hospitali hii kwa kuona umuhimu wa kununua mashine hii kwani nilikuwa nikipata malalamiko kutoka kwa wananchi wangu kwa jinsi wanavyosumbuka pale anatakiwa kupiga Utrasound,”alisema Abood.
Baada ya kuzinduliwa kwa mashine hiyo mbunge huyo alitoa mashine ya kudurufu(printer) yenye thamani ya shilingi 500,000 ili iliwe kusaidia katika kudurufu mara wanapomaliza kufanya vipimo kwa mgonjwa na kuahidi kusaidia kupata mashine nyingine ya Utra-sound.
Akizungumza katika uzinduzi huo mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Morogoro Dk Ritha Lyamuya alisema kuwa kupatikana kwa mashine hiyo kutasaidia kupata majibu kwa usahihi ya wagonjwa watakaopata huduma hiyo.
Dk Lyamuya alisema kuwa mashine hiyo imekuwa ikipima watu 600 hadi 800 kwa mwezi na kwamba kipimo hicho hasa ni muhimu kwa wamama wajawazito na kimekuwa hakina malipo yeyote.
“Magonjwa yanayotumika kupima katika mashine hii ni Moyo,kizazi ,kongoshi,ini,na figo na kilipokuwa hakipo wananchi wetu walipata shida kutokana na gharama wanazotozwa katika hospitali nyingine,”alisema Dk Lyamuya.
No comments:
Post a Comment