Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Maendeleo kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiongea Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani ya Muda wa Wiki Mbili lasivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli Hiyo katiaka ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwajili ya Kusikiliza Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha ia Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2
Wakazi wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame Kaialiyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za wakulima.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katimu wa CCM Kata ya Luhungo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa makini Kero Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugala Kulia.
No comments:
Post a Comment