Friday, 10 January 2014

UANDIKISHAJI WANAFUNZI DARASA LA KWANZA MORO UTATA MTUPU

 Mbunge wa Morogoro Mjini,  Aziz AboodAkizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kihonda wakati wa ziara yake ya kutembelea shule za msingi na sekondari kuangalia zoezi la uandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza.

Mbunge wa Morogoro Mjini,  Aziz Abood  Akipata Maelezo kutoka kwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bungo Mwalimu Luoga aliyevaa Koti Jeupe
 Mbunge wa Morogoro Mjini,  Aziz Abood Akisisitiza jambo wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kutembelea shule za msini.
“ Kwanza ni lazima mtoto aandikishwe kisha iangaliwe namna ya mzazi kumudu kuilipa kwa mwaka halafu umpe michango ya Sh50,000 au zaidi atawezaje,” .
Mjini Morogoro, wazazi wenye watoto wanaoanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kambarage iliyopo Kata ya Chamwino katika Manispaa ya Morogoro jana walipigana  kutokana na kubishania ulipwaji wa mchango wa Sh50,000 .
Vurugu hiyo ilitokea mbele ya Mbunge wa Morogoro Mjini,  Aziz Abood aliyekuwa katika ziara ya kutembelea shule za msingi na sekondari katika jimbo lake ili kujionea uandikishaji wa watoto unavyofanyika.
Wazazi wa watoto ambao walikuwa hawajalipa mchango huo, walikuwa wamejikusanya shuleni hapo.
Mmoja wa wazazi, Hamad Hassan alikiri wazazi kukubaliana michango hiyo kutokana na kikao cha Novemba mwaka jana

No comments:

Post a Comment