Sunday, 5 January 2014

ZAIDI YA BILIONI 12 ZIMEIDHINISHWA KATIKA BARABARA NA MADARAJA MKOA MOROGORO MWAKA 2014

 Wabunge , Mustapha Mkullo wa Kilosa kati, Dk Haji Mponda Ulanga Magharibi, na Abdusalamu Sasi wakifutilia mkutano hu o kwa makini sana.

JUMLA ya shilingi bilioni 12.527.888 zimeidhinishwa  kutumika kwaajili ya kazi za matengenezo ya barabara  na madaraja mkoani Morogoro katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro  Injinia Doroth Mtenga alisema hayo wakati akitoa taarifa katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika Januari 9 mwaka huu mjini Morogoro.
Aidha alisema kuwa fedha hizo zinaunganishwa na  shilingi bilioni 11.277.885 za mwaka wa fedha wa 2012/2013 kukiwa na ongezeko la shilingi bilioni 1,250,000  sawa na asilimilimia 11.08.
Alisema kuwa fedha hizo ni kwaajili ya sehemu korofi , matengenezo ya muda maalumu, matengenezo makubwa ya  madaraja, matengenezo ya kawaida ya barabara na madaraja.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini alisema kuwa pamoja na kupewa fedha hizo lakini pia ni lazima kuweka mikakati ya kudhibiti  uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Alilalamikia tatizo la wafanyabishara wanaoweka bishara zao barabarani na kusababisha magari kusimama hovyo na kuharibu barabara kuwa uchukuliwe hatua.
Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi kupitia idara ya usalama wa barabarani waangalie uwezekano wa kuwa na maeneo maalumu ya kusimamisha magari ili kuepuka kusimamisha hovyo na nivyo kupelekea kuharibu barabara.



 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa bodi ya barabara wakiwa katika mkutano wa 30 uliofanyika Janurai 9 mwaka huu mjini hapa.
 Baadhi ya wajumbe wakifutilia mkutano wa bodi ya barabara.



 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero Jonas Van Zeelanda akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Inocent Karogeries katikati, Celina Kombani mbunge wa Ulanga mashariki, na meya wa manispaa ya Morogoro Amini  katika mkutano huo.
Wajumbe wa bodi ya barabara wakifutilia kikao hicho.

No comments:

Post a Comment