Sunday, 29 March 2015

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WILLIAM LUKUVI ASHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI MOROGORO

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo akikagua karatasi zenye kero za migogoro ya ardhi zilizokuwa zikikabidhiwa kwake kwaajili ya kukabidhi kwa Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi yaliyoandikwa malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana katika ziara yake aliyofanya mkoani humo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi ya malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana katika ziara yake aliyofanya mkoani humo kushoto kwake ni  Mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Abood.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro ambapo kwa siku nzima ya leo alipata fursa ya kusikiliza taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa huo na kisha kupata fursa ya kukusanya karatasi za kero za migogoro ya ardhi kisha kuzikabidhi kwa timu ya wataalamu ambao watazichambua na kutoa mapendekezo kwa waziri jinsi ya kuzitatua pia ameagiza ofisi za Msajili wa Ardhi Kanda ya Mashariki kujengwa na kuhamishiwa Mororgoro.
 Waziri wa Arhdi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akimweleza jambo mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood

No comments:

Post a Comment