Monday, 31 August 2015

PICHA UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA MOROGORO MJINI

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma akimnadi Mgombea Ubunge Wa Jimbo hilo Mh Aziz Abood wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo hilo.Ikumbukwe Mh aziz Abood anatetea Kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo Mara baada ya Kuongoza Jimbo hilo kwa Miaka 5 Kwa mafanikio ya Hali ya Juu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Tuesday, 28 July 2015

AZIZ ABOOD MGENI RASMI MECHI YA MTIBWA SUGAR NA MBEYA CITY


Mgeni rasmi katika tamasha lililoandaliwa na faith baptist church uwanja wa Jamuhuri, hiyo ni match kati ya Mbeya City na Mtibwa.

MBUNGE WA MOROGORO MJINI AKISHIRIKI MICHEZO NA WANANCHI WAKE

 Mbunge wa Jimbo la Morogror Mjini Mh Aziz Abood akiwa jukwani Pamoja na Mashabiki katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kushuhudia Mechi ya Kirafiki kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar
   

Monday, 27 July 2015

WANANCHI WA MOROGORO WAZIDI KUMCHANGIA MBUNGE WAO

 
Mama Mmoja kutoka jimbo la Morogoro Mjini akimchangia Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini katika harakati zake za Kuomba Uteuzi wa Kupeperusha Bendera ya CCM Jimbo la Morogoro Mjini Katika Uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani Utakaofanyika Mwezi October Mwaka Huu
Wakina Mama hawa nao hawakuwa NyumA Kumchangia Mbunge Huyo

Friday, 17 July 2015

WANANCHI WA MOROGORO MJINI WAMNUNULIA FOMU ABOOD ILI AENDELEE KUWA MBUNGE WAO JIMBO MOROGORO MJINI

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Michango ya wanafunzi waliojitokeza Kumchangia Mbunge huyu ili achukue Fomu ya Kugombea tena Ubunge wa Jimbo hilo Kupitia Chama cha Mapinduzi Mara Baada ya Kuridhishwa na Utendaji Kazi wa Mbunge huyo ambaye amefanya Mammbo mengi ya Maendeleo Ikiwemo Kuwalipia Ada zaidi ya wanafunzi 500 Wasiokuwa na uwezo wa Kujilipia ada na wanaoishi Katika Mazingira Magumu
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Kiasi cha Shilingi 50000/= kutoka Kikundi cha Tushikamane Kata ya Kilakala kwa lengo la kumtaka mbunge huyo achukue fomu ya Kugombea Tena Ubunge wa Jimbo Morogoro Mjini .Wanachama wa Kikundi hicho wamesema  wamesukumwa kufanya hivyo Mara baada ya kurishishwa namna Mbunge huyo anavyovisaidia vikundi nvya wajasiriamali wa Jimbo hilo.Hadi sasa Makundi Mbalimbali na wananchi Binafsi wamejitokeza   Kumchangia na Kumshawishi Mbunge huyo kuchukua fomu na kugombea tena awamu nyingine ya ubunge wa jimbo holo..

Friday, 3 July 2015

WAJASIRIAMALI WA LUGALA WA MOROGORO WAMTAKA ABOOD ACHUKUE FOMU YA UBUNGE

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokelewa na Wakazi wa Lugala mara baada ya Mbunge huyo alipowasili kuwatembelea wakazi hao.Katika ziara hiyo wakazi hao walimtaka Mh Abood Achukue Fomu kwajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa Awamu nyingine kwa kuwa Maendeleo aliofanya Kwa kipindi cha Miaka mitano ni Makubwa na hayajawaikufanywa na Mbunge yoyote waliotawala Muda wowote
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwahutubia wakazi wa Lugala
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikabidhi Hundi ya Shilingi laki tano kwajili ya kuwasaidia wajasiriamali hao kuendesha shuguli yao ya ufugaji

AZIZ ABOOD APIGA JEKI UJENZI WA KANISA LA SAMARIA

Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa na waumini wa kanisa la Samaria alipotembelea waumini hao kwajili ya kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Samaria kata ya Mkundi Mkoani Morogoro.Mh Abood alichangia Kiasi cha Shilingi Laki tano kwajili ya ujenzi wa kanisa hilo 
Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akivalishwa mavazi ya Utamaduni ya Kabila la Kimasai
Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akimkabidhi Askofu wa kanisa la Samaria Hundi ya Shilingi Laki tano kwajili ya Ujenzi wa Kanisa la Samaria

Thursday, 2 July 2015

ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI KATA YA MINDU

 Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokelewa na wakazi wa kasanga Mkoani morogoro alipofanya ziara ya kushutukiza kukagua Mradi wa maji wa kijiji hicho.Katika ziara hiyo Mbunge alielezwa kuhusu Mradi wa maji uluizinduliwa na mbio za mwenge uliogarimu zaidi ya  kiasi cha shilingi Milion 400  ambao kwa sasa Maji hayatoki.Mh Mbunge alikagua mradi na kujionea hali halisi na ndipo Mbunge kumpa mkandarasi wa mradi huyo siku saba maji yawe yametoka katika kijiji hicho cha kasanga lasivyo atawashugulikia wahusika
     Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiongozana na wanachi wa Kasanga kwenda kukagua Mradi wa maji wa kijiji hicho.
  Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akishusha nguzo za umeme akishirikiana na wakazi wa Kasanga wakati Mh Mbunge Abood alipotembelea kijiji hicho kwa lengo la kukakua mradi wa maji pamoja na Usambazaji wa Umeme katika kijiji hicho

Monday, 29 June 2015

AZIZ ABOOD AWATEMBELEA KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WA MAZIWA KATA YA KICHANGANI

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood ametembelea kikundi cha wafugaji na wakusanyaji wa maziwa kata ya kichangani mkoani morogoro.katika ziara hiyo mh Mbunge alisikiliza kero zinazokikabili kikundi hicho ambapoa aliwaahidi kuwa nao bega kwa bega namna ya kutatua nchangamoto zinazo wakabili na aliahidi atazitatua mara moja
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea na kikundi cha wajasiriamiali wa maziwa kutoka kata ya Kichangani mkoani Morogoro.

Sunday, 28 June 2015

MBUNGE WA MOROGORO MJINI ACHANGIA MILIONI MOJA KANISA LA FGC

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akitoa hotuba yake kwenye Kanisa la FGC la Mjini Morogoro wakati wa Harambee ya Kuchangisha Fedha kwajili ya Ununuzi wa Vifaa vya Muziki wa Kanisasa Hilo .Mh Mbune akitoa hotuba yake alisisitiza kanisa kuombea Amani pia uchaguzi Mkuu uweze kumalizika kwa Amani na Utulivu.Akieleza Zaidi Mh Abood aliomba kanisa kutokuruhusu wanasiasa Kutumia makanisa kwa lengo la Maslahi yao binafsi
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi Hundi ya Shilingi milioni moja kwa Askofu wa Kanisa hilo ikiwa ni Mchango wake kwenye harambe hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiwa na Katibu wa Kanisa la FGC la Mjini Morogroro.