Sunday, 25 May 2014

SAKATA LA MTOTO ALIYEWEKWA KWENYE BOX MIAKA 4 LAZUA SURA MPYA, NYUMBANI KWA MTUHUMIWA LAKUTWA SHIMO KUBWA LA MAJI

 Nasra akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU  hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 2010.
 Hali ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika box siku tano zilizopita hapo mama  huyo mlezi akimpatia chakula iana ya wali na samaki anaopendelea Nasra. 

 Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa

Petter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali. 
 Habasi zaidi Soma hapo Chini.
 




 SAKATA la Mtoto  aliyeishi katika box kwa miaka 4 sasa limechukua sura mpya baada ya  nyumbani kwa mama mkubwa wake Mariam Said kukutwa  kuna  shimo kubwa lililojaa maji hali inayozidi kuwachanganya wakazi wa mjini hapa.

 Wakiongea na mwandishi wa habari hizi  mwenyekiti wa mtaa wa Azimio  anakoishi mama huyo , Tatu Mgagala alisema Mei 22 polisi walifika mtaani hapo wakiwa na mtuhumiwa huyo  na kukuta mlango umefungwa na kuamua  kuvunja  ili waweze kuingia ndani kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.

Alisema baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mariam walikuta kuna giza nene kutokana na chumba hicho kuzibwa na mabox na hivyo kutoa mabox hayo .

Alisema baada ya kutoa mabox hayo waliona  shimo kubwa lenye maji karibu na eneo  lilipo box alikokuwa  akiishi mtoto huyo  na alipoulizwa mama huyo kulikoni na  kuacha maji ndani huku akijua kuna ugonjwa wa Dengue alidai  maji hayo huyatumia kunawa miguu na mikono usiku kabla ya kulala.

‘’ Ndani ya nyumba hiyo sehemu zote zimesakafiwa isipokuwa eneo hilo ambalo lilichimbwa shimo hilo’’ alisema. Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo imebainika kuwa mariamu na mumewe kwa muda mrefu walikuwa hawajaoga na hivyo kulazimishwa kuoga wakiwa mbaroni .

Kwa upande  wake  mtetezi wa haki za  watoto Petter Mwita alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mei 26 mwaka huu  ni Mariam ,mumewe Mtonga Omari  na baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi.

Alisema  ndani ya nyumba ya mama huyo zikukutwa picha ambazo zinaonyesha kuwa mtoto huyo alikzaliwa akiwa hana ulemavu na kwamba inadaiwa ulemavu huo alipata kutokana na ukatili alikofanyiwa na walezi hao

‘’ Vitendo walivyofanya wote hawa watatu ni vya kikatili na vinatakiwa kupigwa kwa nguvu zote nah ii itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii.

Alisema baadhi ya mitandao ya kijamii ilivumisha kuwa mtoto huyo alinyanyasika na mama yake mkubwa huyo kwa madai kuwa mama yake mzazi alikufa na ugonjwa wa Ukimwi  ambapo alisema suala hilo kwa mtoto huyo halipo kwani tayari alishafanyiwa kipimo hicho na kubaini hana ugonjwa huo.

Hata hivyo alisema kwa sasa wamemtafuta mama mlezi wa Mtoto huyo kwaajili ya kumuhudumia katika huduma zote na anlipwa kwa kazi hiyo.

Naye Josephina Joel mama ambaye kwa sasa ndiye anamlea mtoto huyo alidai yeye amechukuliwa kutoka katika kambi ya kulelea wazee Fungafunga ya mjini hapa na kwamba anajua uchungu wa watoto hivyo kwake anaona hakuna changamoto zozote anazopata kwa mtoto huyo.

‘’ Mimi niliachwa na mume wangu naishi  Fungafunga nalelewa na Ustawi wa jamii kwangu kumlea mtoto huyo nachukulia kama mjukuu wangu na nafurahia na sioni shida yeyote’’ Alisema.

Aidha alisema mtoto huyo hupendela kula chipsi mayai, wali nyama au samaki pamoja na juice huku akionyesha kukataa ugali wala maziwa.

Mtoto huyo kama kitu hataki anafumba macho, kwa mfano ukimwambia nikupe ugali anakataa, au maziwa , lakini pia hapendi kuoga na ukimwambia kuoga au kula vyakula asivyotaka anakwambia badae’’ Alisema

Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kufika nyumbani kwa  Mvungi Kihonda eneo la Maduka kumi anakoishi na mkewe wa ndoa  kwa lengo la kutaka kujua jinsi huyo mke  alivyochukulia jambo hilo na kuwafukuza waandishi wa habari kwa madai ya kuwa wakaandike wanavyojua wao.

‘’ Ehe waandishi wa habari mnataka nini tena kwangu uwiiii, mimi sijui chochote, ondokeni,  huku akiondoka kueleka sebuleni waliko mgeni wake aliyemtmbulisha kama wifi yake huku akimwambia kwa lugha ambayo ilisikika kwa neno   lililoashiria wandishi wa habari hao’’ Alisema


 Hata hivyo  waandishi wa habari walifika nyumbani hapo   nao wakiwa nyuma yake wakarudi naye hadi eneo alipo  wifi yake na kujaribu kudadisi zaidi jambo  bila mafanikio zaidi ya kutawala kimya kwa muda wa dadki kumi na ndipo alipoohoji tena kuwa wanataka nini.

Hata hivyo mama huyo ambaye anaonekana ni mjamzito alionekana kupandisha pumzi na kushusha hali iliosababisha kushindwa kuongea na hivyo waandishi hao kuamua kuondoka kurejea mjini.

Kamanda wa polisi mkoani hapa alithibitisha kukamatwa kwa baba wa Nasra Said  na kwamba yuko nje kwa dhamana na aatafikishwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wezake Mei 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment