Saturday, 10 May 2014

WAZIRI GHASIA ASEMA IPO HARUFU YA RUSHWA KATIKA UPANGAJI NA UHAMISHO WA WALIMU, ATAKA ISHUGHULIKIWE HARAKA

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia  akioongea na wajumbe wa baraza la wizara hiyo wakati wa kujadili bajeti ya wizara yake uliofayika jana mjini hapa





 Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakisikiliza kwa makini mkutano huo wa baraza jana

 Wajumbe wa baraza hilo .


Habari zaido soma hapo chini


Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia amesema  upangaji wa vituo kwa watumishi wapya hususani walimu ni eneo moja wapo lenye hafuru ya Rushwa  na kutaka watumishi wanaotuhumiwa kuchukuliwa hatua.

 Alisema eneo hilo limeanza kutoa dalili si njema na kuongeza kuwa ni vyema wakachukua tahadhari na kujiridhisha kwa kubaini mapungufu ya kiutendaji katika eneo hilo na kuhakikisha wanaziba mianya ya rushwa.

Alisema hayo Mei 5 mwaka huu wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa TAMISEMI linaoendela mkoani Morogoro.

Aidha alimuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuchukua hatua za haraka  dhidi ya watumishi  wanaotumiwa kwa rushwa au kutoa huduma kwa upendeleo na wale wanaoshirikiana na maafisa katika mamlaka za serikali za mitaa kuzihujumu mamlaka hizo.
Waziri Ghasia alisema ofisi hiyo imepigiwa kelele kwa muda mrefu na wadau mbalimbali  juu ya vitendo vya rushwa,hivyo ni wakati sasa kwa wizara hiyo kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mifumo ya
‘’ Ni muda muafaka sasa kuhakikisha tuhuma hizo zinakwisha, kwa kuchukua hatua madhubuti za kuborsha mifumo ya utendaji kazi katika eneo hili’’ Alisema

Alisisitiza juu ya kuimarisha usimamizi na ufutiliaji wa matumizi ya fedha  kupitia MSM  kupitia mifumo ya fedha waliokwishawekeza (Epcor/IFMS) ambapo alisema dalili zinaashiria ufuatiliaji kupitia mifumo hiyo bado ni hafifu.

Katibu mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne  Sagini aliwataka watumishi wa ofisi hiyo    kujadili changamoto zinazoikabili ofisi hiyo ili ziweze kutatuliwa na waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kikao cha baraza la wafanyakazi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa kinafanyika mjini Morogoro na kimelenga kujadili bajeti ya wizara hiyo kabla ya kwenda kujadiliwa kwenye bunge la bajeti mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment