Tuesday, 6 May 2014

KIWANDA CHA NGUO CHAAGIZWA KUINGIA KATIKA MFUMO WA MAKAA YA MAWE JUMLA

 WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith Malenge  alipotembelea kiwanda cha Twenty Firts Centuary kuangalia matumizi ya makaa ya mawe badala ya magogo ya miti waliokuwa wakitumia zamani na kupigwa marufuku na serikali.
 Waziri huyo akiangali maeneo mbalimbali ya mabwa ya maji katika kiwanda  hicho.
 Waziri huyo akiangali maji yanayotoka kiwandani humo ambayo yanakemikali yanaingia katika mto Ruvu ambayo yanamadhara kwa binadamu.
WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith Malenge amekiagiza kiwanda cha Twenty first centuary kuhakikisha ifikapo mwezi Agosti mwaka huu wawe wamebadilisha mfumo wa maboiler ya kutumia nishati ya magogo ya miti na kuingia katika mfumo wa makaa yam awe.
Alisema hayo jana wakati alipotembela kiwandani hapo kuangalia jinsi ya uendeshaji wa kiwanda na kujionea mfumo mzima wa uhifadhi wa mazingira kiwandani hapo.
Alisema kuwa pamoja na juhudi walizofanya kiwanda hicho kuacha kutumia magogo ya miti ambayo yalikuwa yakiharibu mazingira na kuingia katika mfumo wa makaa ya mawe lakini bado mfumo wa vifaa  vya kuchemshia maji upo katika mfumo wa kutumia magogo.
Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa vumbi linalosambaa hewani na hivyo kusababisha kero kwa wananchi wa maeneo jirani na hapo.
‘’ sasa ni lazima ikifika mwezo wa nane mbadilishe maboiler yenu yawe katika mfumo wa makaa yam awe ili kuondokana na usumbufu’’ Alisema Waziri huyo.
Hata hivyo waziri huyo alishauri faini zinazotozwa na NEMC zingetumika kuboresha mabwawa ya maji yanayotumiwa na viwanda vya nguo na ngozi vya mjini hapa ili kuweka mazingira safi.
‘’ Mimi naona hizi faini mnazotoza mngezipeleka kuhakikisha mnaboresha mabwawa hayo ili kuondokana na adha ya maji kujaa  na kufurika nje ya mabwawa na kusababisha adha kwa wananachi wa karibu na  hata kuingia mtoni na badae kuleta madhara kwa watumiaji wa mto huo ‘’ Alisema
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi alipongeza juhudi zilizofanywa na vyombo vya habari mkoani hapa za kuhakikisha wanaripoti btaarifa juu ya matumizi ya magogo ya miti kwa kiwanda hicho hadi kufikia sasa matumizi hayo yamechwa.
‘’ Kweli serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya habari  kuhakikisha zoezi la matumizi ya  magogo limesitishwa sasa’’ alisema Amanzi.

No comments:

Post a Comment